VIKAO VYA KUSIKILIZA HOJA YA KUMBANDUA MAMLAKANI WAZIRI WA KILIMO MITHIIKA LINTURI VINAENDELEA

Vikao vya kusikiliza hoja ya kumbandua mamlakani waziri wa kilimo Mithiika Linturi vinaendelea ambapo waziri huyo amehojiwa akiwa wa kwanza na kukanusha madai ya kuhusika na sakata ya usambazaji wa mbolea gushi na madai kwamba ndiye aliyeidhinisha kusambazwa kwa mbolea hiyo kwa wakulima. Vile vile Linturi ameongeza kwamba hafai kuwajibishwa kwa sakata hiyo kwa kuwa ni taasisi tofauti zinazohusika na mbolea ya ruzuku wala sio afisi yake.