OWALO, KISIANG’ANI WAITWIKA CAK JUKUMU

Waziri wa mawasiliano na uchumi wa kidijitali Eliud Owalo na katibu wake mkuu Edward Kisiang’ani, wameitaka mamlaka ya mawasiliano CAK kuwa mstari wa mbele katika kutekeleza ajenda ya serikali katika nyanja ya kidijitali.
Wakizungumza wakati wa uzinduzi wa ruwaza ya mamlaka hiyo katika kipindi cha miaka mitano ijayo, wamesema kuwa CAK imo katika nafasi nzuri kuhakikisha serikali inaafikia malengo yake ya kidijitali.
Aidha, Kisiangani ameitaka CAK kubuni sheria za udhibiti ili kuhakikisha ushindani kwa njia ya usawa.
Imetayarishwa na: Antony Nyongesa