#uncategorized

POLISI WA KENYA KUELEKEA HAITI MWEZI HUU

Maafisa wa polisi wa Kenya wanatarajiwa kuelekea nchini Haiti kukabili makundi ya uhalifu kabla ya ziara rasmi ya Rais William Ruto mwishoni mwa mwezi huu nchini Marekani.

Kwa mujibu wa katibu mkuu katika wizara ya mambo ya kigeni Kipkorir Sing’oei, kikundi cha kwanza cha maafisa hao ambao ni takribani 200, kinatarajiwa kuondoka nchini kati ya Mei 18 na Mei 22.

Ikulu ya Marekani imethibitisha kwamba Rais Joe Biden na mkewe Jill Biden, watakuwa wenyeji wa Rais William Ruto na mkewe Rachel Ruto kwa ziara ya kitaifa Mei 23, kuadhimisha miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia baina ya Kenya na Marekani.

Imetayarishwa na: Antony Nyongesa

KALONZO AWAONYA WABUNGE WA AZIMIO

SENETI YAMHOJI WAZIRI MVURYA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *