RUTO ATANGAZA USHIRIKIANO NA UGANDA

Rais William Ruto amesema kuwa maifa ya Kenya na Uganda yatashirikiana katika masuala mbali mbali ikiwemo biashara ili kuimarisha uchumi na maendeleo, mbali na kukabili ugaidi na athari za mabadiliko ya hali ya anga.
Kwa upande wake, Rais Yoweri Museveni amempongeza Ruto kwa kudumisha uhusiano baina ya Kenya na Uganda kama njia mojawapo ya kukabili changamoto zinazokumba jumuiya ya Afrika Mashariki na Bara la Afrika kwa jumla.
Museveni yuko nchini kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili.
Imetayarishwa na: Antony Nyongesa