SERIKALI IMEPIGA MARUFUKU UNGA WA MAHINDI WA SHERE

Wizara ya afya imetoa tahadhari kuhusu aina moja ya unga wa mahindi wenye viwango vya juu vya sumu ya Aflatoxin.
Kaimu mkurugenzi wa wizara ya afya dkt Patrick amoth anasema unga wa sherehe una viwango vya aflatoxin Zaidi ya vile zinavyokubalika hivyo sio salama kwa matumizi ya umma.
Amoth vile vile ametoa wito kwa umma kutonunua unga huo na wafanyibiashara kutouza.
Wizara ya afya vile vile imeagiza ukaguzi kufanywa kwa bidhaa nyingine sokoni kama vile njugu kubainisha viwango vya aflatoxin ilikuzuia madhara.
Imetayarishwa na: Janice Marete