#uncategorized

KONGAMANO LA LIMURU III LITAFANYIKA LEO HII

Viongozi mbali mbali wa kisiasa, kidini na wasomi wa eneo la mlima kenya wanatarajiwa kukongamana leo hii katika ukumbi wa jumuia eneo la kabuki katika mkutano maarufu Limuru 3 kujadiliana maswala mbali mbali yanayolikumba eneo hilo.

Licha ya kuwapo kwa hisia kinzani baina ya viongozi wa eneo hilo kuhusu kufanyika kwa mkutano huo, waandaji wanasisitiza kwamba mkutano wa leo utatumika kujadili maswala yanayowakumba wakaazi wa eneo la mlima kenya kisiasa,kiuchumi nahata kimaendeleo na kisha kuafikiana maamuzi muhimu.

Katibu mkuu wa chama cha jubilee Jeremiah Kioni ,kinara wa KNAC kenya Martha Karua na aliyekuwa gavana wa laikipi Nderitu Murithi ambao wamehusika pakubwa katika matayarisho ya kongamano hilo wameitaja mikutano ya Limuru 1 na 2kuwa inayojulikana kwa kufanya maamuzi yaliyoelekeza eneo hilo kisiasa na maendeleo na kwamba Limujru 3 itafanya vivyo hivyo.

Imetayarishwa na: Janice Marete

CAK: TATIZO LA INTANETI KUENDELEA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *