#Business #Local News

GAVANA NATEMBEA AWAHIMIZA WAKAAZI KUCHUKUA MIKOPO KUJIENDELEZA KIBIASHARA

Gavana wa kaunti ya Transnzoia George Natembea amewarai wakaazi wa kaunti hiyo kutumia fursa zilizopo katika benki kuchukua mikopo ili kufanya biashara na serikali kupitia njia mbali mbali za kibiashara.


Akiwahutubia wanahabari baada ya kufungua rasmi tawi la 21 la benki ya kingdom mjini Kitale, Natembea amesema tayari serikali imezindua hazina ya nawiri ya kima cha shilingi milioni 100 ili kuwezesha takribani makundi 250 ya kina mama,vijana na watu wenye walemavu ili kujiendeleza kiuchumi.


Kwa upande wake afisa mkuu mtendaji wa benki ya kingdom Anthony Mburu amesema kuwa wakulima wanaweza kuchukua mikopo na kuendeleza kilimo biashara.

Imetayarishwa na: Janice Marete

‘TULIPE USHURU TUJITEGEMEE’ ASEMA RUTO

UHABA WA MAJI WAKUMBA MJI WA HOMA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *