COCA-COLA YATANGAZA MIPANGO YAKUWEKEZA KSH23B NCHINI KENYA

Kenya imetia Saini kwa mpango wa upanuzi wa uwekezaji wa shilingi billioni 22.8 na kampuni ya Coca-Cola pale ambapo ushirikiano huo utadumu kwa miaka mitano ijayo.
Katika taarifa Msemaji wa Ikulu Hussein Mohamed ametangaza hayo baada ya Rais William Ruto, akiwa na viongozi wengine wa Kenya, kutembelea makao makuu ya kampuni hiyo huko Atlanta, Georgia, nchini Marekani.
Baada ya kutia Saini mkataba huo Katibu wa Baraza la Mawaziri la Biashara na Uwekezaji Rebecca Miano amesema kuwa ushirikiano huo utachukua jukumu muhimu katika kuunda nafasi za kazi na kukuza uchumi wa Kenya.
Kwa upande wake gavana wa Nairobi Johnson Sakaja ameelezea matumaini kuwa hatua hiyo itaunda nafasi za ajira kwa wakazi wengi wa Nairobi.
Mkutano huo ulikuwa sehemu ya ratiba ya Rais katika ziara yake ya wiki moja Marekani.
Imetayrishwa na: Maureen Amwayi