#Business #Local News

‘JSS TEACHERS WATAAJIRIWA KWA KANDARASI YA KUDUMU’ NDINDI NYORO ASEMA

Serikali itawaajiri kwa kandarasi ya kudumu walimu wa sekondari ya msingi JSS ambao kwa sasa wako katika kandarasi ya muda na masomo ya nyanjani.

Haya ni kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati ya bajeti katika bunge la kitaifa Ndindi Nyoro, amabaye amedokeza kwamba kamati yake imelijumuisha swala hilo katika bajeti ya tume ya huduma za walimu TSC katika mwaka wa kifedha wa 2024-2025.

Kauli ya nyoro inajiri wakati ambapo kumekuwa na mvutano baina ya TSC na walimu wa JSS kuhusu kuaajiriwa kwa kandarasi ya kiudumu kufuat5ia uam uzi wa mahakama Kando ya hayo  nyoro katika maojiano na kituo kimoja cha runinga hapa nchini amepuuzilia mbali madai kwamba mpango wa chakula shuleni umeodolewa kwa kuwa haukujumuishwa kwenye makadirio ya bajeti yam waka wa 2024-2025 wa kifedha.

Kwa mujibu wa nyoro shilingi bilioni 4 ambazo zimekuwa zikitengewa mpango wa chakula shuleni zitatengewa idara nyingine ya serikali ambayo imetwikwa jukumu la kusambaza chakula shuleni.

RUTO: SIASA MBAYA IMETUGHARIMU KAMA TAIFA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *