#Local News

RUTO ATIA SAINI MKATABA KUJENGA BARABARA YA NAIROBI-MOMBASA

Rais William Ruto ametia saini mkataba wa mradi wa kihistoria wa ujenzi wa barabara ya moja kwa moja baina ya Nairobi na Mombasa ambao utatekelezwa na kampuni ya kimarekani kwa gharama ya shilingi bilioni 477.

Mradi huo ambao umepewa jina la USAHIHI TOLL ROAD utatekelezwa kwa ushirikiano baina ya kampuni hiyo na Mamlaka ya barabara kuu nchini KeNHA.

Barabara hiyo kuu ambayo itakuwa na barabara 6 na urefu wa kilomita 400, itakamilishwa ndani ya kipindi cha miaka mitatu na minne ijayo.

Imetayarishwa na: Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *