KNUT YAAMRISHA WALIMU WA JSS KUREJEA KAZINI

Chama cha kitaifa cha walimu KNUT kimewaagiza walimu wa shule za sekondari ya msingi JSS wanaogoma kurejea kazini.
Katibu mkuu wa KNUT Collins Oyuu anasema chama hicho kiko tayari kufanya mazungumzo na tume ya huduma za walimu TSC kushughulikia malalamiko yao amabyo yamekuwa yakiibuliwa wakisema kwamba wanafunzi wanaangaika na wanasalia nyuma kimasomo.
Oyuu amesema tayari TSC imekubali kuondoa barua walizokuwa wameandikiwa baadhi ya walimu kutaka kueleza ni kwa nini wasichukuliwe hatua kwa kukosa kurejea kazini.