OMBOKA AWATAKA WABUNGE KUIDHINISHA FEDHA ZA KUWAAJIRI WALIMU WA JSS
Mwenyekiti wa chama cha walimu wa shule za upili na vyuo vya kadri KUPPET Jeremiah Omboka Milemba amewarai wabun ge kuidhinisha fedha za kuwaajiri walimu wa sekondari ya msingi kwa kandarasi ya kudumu katika bajeti ya mwaka 2024.
Kwa mujibu wa Milemba hatua hiyo itasitisha maandamano ya walimu ambayo yanatatiza utekelezwaji wa mtaala wa elimu CBC katika shule za umma.
Milemba ambaye pia ni mbunge wa Emuhaya amesisitiza kwamba kutengwa kwa fedha hizo kuitawezesha tume ya huduma za walimu TSC kuwa fedha za kuwaajiri walimu wa kutosha hatua ambayo kulingana naye itainua viwango vya elimu nchini.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































