VIONGOZI WA AZIMIO WAENDELEA KUKASHIFU MSWADA WA BAJETI

Viongozi wa azimio wanaendelea kukashifu mswada wa fedha wa mwaka 2024-2025 wakidai kwamba wabunge hawana uwezo wa kuwalinda wakenya dhidi ya kuongezwa kwa kodi ya bidhaa muhimu
Katika mahojiano na runinga moja humu nchini hapo jana kiongozi wa Democratic Action Party DAP kenya Eugene Wamalwa amesema rais William Ruto amepuuza kauli za wakenya na viongozi mbali mbali kuhusu kuongezwa kwa kodi ya bidhaa muhimu kama vile mafuta ya kupikia na mkate
Wamalwa vile vile amesisitiza kwamba viongozi wa upinzani wataongoza maandamano iwapo serikali haitalishawishi bunge la kitaifa kupitisha mswada huo anaodai kwamba unalenga kujwakandamiza wakenya zaidi hasa walio na mapato ya chini.
Imetayarishwa na Janice Marete.