#Local News

KAUNTI KUPOKEA MGAO WA BILIONI 400

Serikali za kaunti sasa zinatarajia kupokea mgao wa shilingi bilioni 400 ambayo ni juu zaidi tangu kuanzishwa kwa mfumo wa ugatuzi

Hatua hiyo inafuatia makubaliano yaliyoafikiwa baina ya bunge la kitaifa na seneti kupitia kamati maalum ya upatanishi ambayo iliteuliwa kutafuta mwafaka

Awali bunge ilisisitiza kwamba kaunti zinapaswa kupokea mgao wa shilingi bilioni 361 huku seneti ikipendekeza kaunti zipate mgao wa shilingi bilioni 415

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kiamati ya bajeti katika bunge la kitaifa ndindi nyoro ambaye aliwakilisha bunge la kitaifa katika mazungumzo hayo ameitaka serikali za kaunti kuwajibikia fedha ambazo zitapokea kwani zitakuwa ni shilingi bilioni 15 zaidi ya walizopokea mwaka jana ambazo ni bilioni 385

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *