WAFUNGWA KWENYE KESI YA THUO KUHUKUMIWA JUNI

Wafungwa sita waliopatikana na hatia ya mauaji ya aliyekuwa mbunge wa Juja George Thuo watahukumiwa tarehe 21 mwezi ujao, huku mjane wa marehemu Judy Thuo akiiomba mahakama kuwapa adhabu kali.
Jaji Roselyn Korir amesema atatoa uamuzi wake kuhusu hukumu ambayo iataashiria kukamilika kwa kesi ya mauaji ya Thuo
Wafungwa hao ni Paul Wainaina Boiyo, msaidizi wa Thuo Christopher Lumbazio Andika, wacheza santuri Andrew Karanja Wainaina na Samuel Kuria Ngugi, Esther Ndinda Mulinge na Ruth Watahi Irungu
Imetayrishwa na Antony Nyongesa