KOCHA ODHIAMBO HAJARIDHISHWA NA MATOKE YA KIKOSI CHAKE
Kocha mkuu wa Equity Dumas Carrey Odhiambo hajafurahishwa na Mchezo wao katika msimu wa kawaida huku timu hiyo ikielekeza fikira zake kwa mchujo ambao utakamilika kwa uteuzi wa bingwa wa michuano ambayo inakuja.
Kulingana na Odhiambo, Dumas hawakufanya vyema katika mechi kadhaa, hivyo basi kuporomosha pointi zao . `
Wanabenki hao waliwazaba Ulinzi Warriors 61-57 mnamo Ijumaa kabla ya kuwalaza ANU Wolfpacks 53-59 Jumapili kwenye uwanja wa Nyayo Gymnasium, Nairobi
Kwingineko, kocha mkuu wa ANU Wolfpacks na Panthers Michael Oluoch anasema timu zake hazikucheza vyema wikendi na itabidi kurekebisha makosa yaliyofanywa kabla ya mechi ya mchujo ya mwisho.
ANU Panthers ilipoteza 27-67 na 43-64 na Equity Hawks, USIU Flames Jumamosi na Jumapili mtawalia, kwenye ligi kuu ya wanawake huku ANU Wolfpacks ikipoteza 38-51 na 53-59 na USIU Tigers na Equity Dumas Jumamosi na Jumapili mtawalia mechi za ligi kuu.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































