KESI YA MAUAJI YA SHARON OTIENO INAENDELEA KUSIKILIZWA

Mpelelezi mkuu wa mauaji ya aliyekuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Rongo Sharon Otieno anatarajiwa kuhojiwa leo hii na upande wa utetezi katika kesi ya mauaji inayomkabili aliyekuwa gavana wa Migori Okoth Obado.
Mnamo mei kumi mpelelezi aliiambia mahakama kwamba msaidizi wa Obado Michael Oyamo alipanga matukio yaliyosababisha mauaji ya Sharon.
Nicholas Olesena amesema kwamba katika siku ya mauaji Oyamo aliwapeleka Sharon na mwadishi wa habari kwenye gari lililokuwa likiwasubiri umbali wa mita 300 kutoka hoteli ya Grace huko Rongo baada ya mkutano mfupi.
Mwanahabari huyo ambaye alifanikiwa kutoroka kwenye gari hilo anadaiwa kutoa ripoti ambayo wachunguzi wanategemea kuwafungulia mashtaka washukiwa hao.