#Football #International #Sports

CHELSEA ILIIMARIKA MIKONONI MWANGU ASEMA MAURICIO POCHETTINO

Mauricio Pochettino alisema Chelsea imeonyesha maboresho makubwa  katika msimu wake mmoja kama meneja katika maoni yake ya kwanza hadharani tangu kuondoka kwake Stamford Bridge.

Muargentina huyo aliondoka katika klabu hiyo kwa makubaliano mwezi uliopita licha ya kumalizika kwa msimu wenye misukosuko ambapo walitumia muda mwingi wa kampeni kudorora katikati mwa jedwali la Ligi ya Premia.

The Blues walishinda michezo yao mitano ya mwisho na kumaliza nafasi ya sita na kupata nafasi ya kushiriki Ligi ya Mikutano ya UEFA, pia kuiinga fainali ya Kombe la Ligi na nusu fainali ya Kombe la FA. Siku ya Jumatatu, Chelsea ilimteua kocha wa Leicester Enzo Maresca kuwa mrithi wa Pochettino. kwa mkataba wa miaka mitano.

Kocha huyo wa zamani wa Tottenham na Paris Saint-Germain alisema timu hiyo imesonga mbele baada ya kumaliza katika nafasi ya 12 kwenye Ligi ya Premia msimu wa 2022/23.

Imetayrishwa na Nelson Andati

CHELSEA ILIIMARIKA MIKONONI MWANGU ASEMA MAURICIO POCHETTINO

MALIKI WATAMBA BUNGOMA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *