CBK: RIBA YA MIKOPO KUSALIA
Wakopaji wa mikopo wamepata afueni baada ya Benki Kuu ya Kenya (CBK) kutangaza kwamba haitaongeza kiwango cha riba, bali itabakia asilimia 13,
CBK imesema msimamo wa sasa wa sera ya fedha umepunguza vitisho vya mfumuko wa bei, licha ya benki kuendelea kupunguza viwango vya mikopo kwa wateja, huku wengi wa wakopaji wakiendelea kushindwa kulipa mikopo hiyo
Katika taarifa, CBK imesema mfumuko wa bei unatarajiwa kupungua zaidi na hivyo kuwapa afueni kubwa kwa Wakenya walio na uhaba wa pesa.
Imetayarishwa na Maureen Amwayi
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































