GACHAGUA HAJAFURAHISHWA NA SERIKALI KUUNGA MKONO RAILA AU – SENETA MAANZO

Seneta wa Makueni Dan Maanzo amesema kuwa Naibu wa Rais Rigathi Gachagua amekerwa na hatua ya serikali kuunga mkono azma ya Raila Odinga kuwa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC).
Kwa mujibu wa Maanzo mzozo uliopo kati ya Gachagua na serikali umeongezeka kiasi cha yeye kuchukia kila hatua ambayo serikali hufanya
Maanzo amebainisha kuwa masaibu ya Gachagua ni matokeo ya matendo yake mwenyewe tangu alipoanzisha mazungumzo ya siasa za kikabila alipokuwa akitoa matamshi ya wanahisa wenye utata akisisitiza kwamba baadhi ya jamii zitanufaika na serikali kuliko nyingine
Imetayarishwa na Janice Marete