#Sports

NYOTA WA TOTTENHAM APORWA

Nyota wa Tottnham Hotspurs, Yves Bissouma alishawishiwa na genge lililojifanya kama mashabiki wakitaka kujipiga picha pamoja na yeye kabla ya kupigwa mabomu ya machozi na kuibiwa.

Kiungo huyo wa kati wa Spurs, 27, aliporwa saa yake ya kifahari ya Richard Mille yenye thamani ya pauni 260,000 [Zaidi ya shilingi za Kenya milioni 43] alipowasili katika hoteli moja ya Ufaransa akiwa na mpenzi wake asubuhi ya Jumapili.

Watu wawili waliojifunika nyuso zao pia waling’oa pete tatu za almasi kwenye vidole vya mpenzi wake ambaye hajatambuliwa walipokuwa wakijaribu kuingia katika hoteli ya kifahari huko Cannes mwendo wa saa nne asubuhi.

Maafisa katika eneo la mapumziko la French Riviera walielezea jinsi wawili hao walivyokabiliwa na wahalifu hao, huku Bissouma akiwaambia polisi alijaribu kukimbilia ndani ya mali hiyo ya nyota tano – lakini milango yake ilikuwa imefungwa.

Bissouma na mpenzi wake walishtushwa na kufadhaishwa sana na shambulio hilo na wametoa wito kwa polisi kufanya uchunguzi wa kina.

Imetayarishwa na Nelson Andati

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *