KAMPUNI KADHAA ZATISHIA KUSITISHA UFADHILI WA MIRADI KENYA

Kampuni kadhaa na ambazo zinafadhili miradi mbali mbali humu nchini zimetishia kutofadhili miradi ya mabilioni ya fedha iwapo mswada wa fedha wa 2024-25 utapitishwa jinsi ulivyo
Kwa upande mwingine washikadau katika sekta ya mazingira na mawasiliano wameonya kwamba itakuwa vigumu kuendeleza shughuli zao nchini kufuatia kuongezwa kwa kodi katika huduma za mawasiliano
Kufikia sasa mashirika na kampuni 106 zimewasilisha hoja zao mbele ya kamati ya bunge ya fedha na mipango katika vikao vya umma vinavyoendelea huku mashirika mengine 40 yakiratibiwa kuwasilisha hoja zao mbele ya kamati hiyo
Imetayarishwa na Janice Marete