MBUNGE KANGOMBE AKANUSHA MAUAJI

Mbunge wa Gatundu Kusini Gabriel Kagombe ameachiwa huru kwa dhama ya shilingi milioni 1 pesa taslimu au dhamana ya shilingi milioni 2 na mdhamini wa kiasi sawa na hicho baada ya kukana mashtaka ya mauaji dhidi yake.
Katika kesi hiyo, Kagombe anatuhumiwa kumpiga risasi hadi kufa mhudumu wa boda boda kwa jina David Nduati mnamo tarehe 17 mwezi jana katika eneo la Thika kaunti ya Kiambu, baada ya malumbano ya kisiasa baina ya makundi pinzani.
Jaji wa mahakama kuu mjini Machakos Francis Olel, amesema kesi hiyo itatajwa tarehe 17 mwezi ujao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa