HATUSHINDWI KUTUMIA PEA; MAGAVANA

Baraza la magavana limeendelea kumlaumu mdhibiti wa bajeti kwa kuchelewesha mgao wa fedha za kaunti.
Kwa mujibu wa naibu mwenyekiti wa baraza la magavana Ahmed Abdulai shughuli za maendeleo katika kaunti zimelemazwa kufuatia kucheleweshwa kwa fedha za kaunti.
Abdulai ambaye pia ni gavana wa kaunti ya wajir amepuuzilia mbali madai ya mdibiti wa bajeti Margaret Nyakango kwamba kaunti nyingi ushindwa kutumia fedha zilizotengewa na kusema hilo usababishwa na kuchelewa kwa fedha hatua ambayo uwanyima fursa magavana ya kupangia fedha hizo.
Imetayarishwa na Janice Marete