WAFANYABIASHARA WADAI KODI INAMEZWA NA UFISADI

Huku zoezi la kupokea maoni kuhusu mapendekezo ya mswada wa kifedha wa mwaka 2024-25 likitarajiwa kukamilika hii leo, jamii ya wafanyabiashara chini ya muungano wao wa PKF wamesikitishwa na baadhi ya mapendekezo hayo, wakisema yatalemaza sekta muhimu kama vile kilimo na uchukuzi.
Wakiongozwa na Michael Mbungu kwenye kikao na wanahabari jijini Nairobi, wafanyabiashara hao wamewataka wabunge kkuangusha mswada huo, na kupendekeza kukabiliwa kwa ufisadi kama njia mojawapo ya kuhakikisha ushuru unaotozwa unamfaidi mwananchi.
Kwa upande wake, Kevin Chege ambaye ni masimamizi wa kitengo cha ushuru katika muungano huo, amepinga pendekezo la kubatilisha sheria inayozuia kutozwa ushuru baadhi ya bidhaa za kilimo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa