WAKENYA HAWANA IMANI NA RUTO, GACHAGUA- UTAFITI
Utafiti wa shirika la Infotrak umeonyesha kwamba wakenya hawana imani na utendakazi wa Rais William Ruto na NAibu Wake Rigathi Gachagua Pamoja na baraza la mawaziri, Ruto na Gachagua wakipata alama ya D.
Kwenye utafiti huo uliofanywa kati ya tarehe 23- 29 mwezi mei mwaka huu, Waziri wa usalama Kithure Kindiki ameorodheshwa kama Waziri bora kwa alalam 60, mwenzake wa michezo Ababu Namwamba akipata alama 51, huku Mithika Linturi wa kilimo akiorodheshwa wa mwisho kwa alama 39 ambayo ni E.
Akitoa matokeo hayo hii leo, mkuu wa utafiti wa Infotrak Johvine Wanyingo amesema bunge, idara ya mahakama na upinzani pia umepewa alama ya D kwenye utafiti uliojumuisha wakenya 1,700 kutoka kaunti zote 47
Imetayarishwa na
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































