KENYA KUPOKEA SHILINGI BILIONI 126.2 KUTOKA KWA IMF

Taifa la kenya limefikia makubaliano ya kiwango cha wafanyakazi na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), kutoa malipo ya dola milioni 976, ikiwa ni sawa na shilingi bilioni 126.2.
Mpango huo ni sehemu ya sera na mageuzi ya kina yanayohitajika ili kukamilisha ukaguzi wa Mpango wa Hazina ya maendeleo ya taifa hili
Kulingana na IMF kuidhinishwa kwa Bodi yake ya Utendakazi kuhusu kupitishwa kwa Mfumo wa pili wa Ustahimilivu na Uendelevu wa taifa la Kenya utahakikisha upatikanaji wa haraka wa dola milioni 120 kiwango sawa na shilingi bilioni 15.5.
IMF, imeitaka serikali ya Kenya kuhakikisha inaweka mikakati kabambe ili kuhakikisha kuwa ina uwezo wa kulipa deni
IMF pia inataka marekebisho ya mswada wa fedha katika bajeti ya mwaka 2024/2025 ili kuweka mikakati ya kuongeza mapato.
Imetayarishwa na Maureen Amwayi