AFARIKI AKIFARIJI
Familia moja katika kaunti ndogo ya Bondo ina huzuni baada ya jamaa yao kuzimia na kufariki alipokuwa akitoa ushahidi katika kesi ya urithi wa ardhi katika mahakama ya Bondo.
Marehemu amekimbizwa katika hospitali ya kibinafsi na familia yake, ambapo ameaga dunia alipokuwa akipokea matibabu.
Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Siaya Cleti Kimaiyo amesema kisa hicho kimeripotiwa katika kituo cha polisi cha Bondo na Dick Ochiel, msimamizi wa mahakama ya Bondo.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































