USHURU WA MKATE WATUPILIWA MBALI

Serikali ya Kenya Kwanza imetupilia mbali mapendekezo makuu ya ushuru ambayo yamezua taharuki miongoni mwa Wakenya
Tangazo hilo linajiri baada ya Rais William Ruto kuandaa mkutano wa kundi la wabunge katika Ikulu ya Nairobi hii leo
Katika kikao na wanahabari baada ya mkutano wa PG, wandani wa rais Ruto wamesema mapendekezo hayo yametupiliwa mbali kufuatia zoezi la ushirikishwaji wa umma ambalo lilishuhudia Wakenya wakiibua upinzani dhidi yao
Miongoni mwa mapendekezo yaliyorekebishwa ni ushuru wa mkate, gari na ushuru wa mazingira
Imetayarishwa na Janice Marete