WAANDAMANAJI WA KUPINGA MSWADA WA FEDHA WAKAMATWA NAIROBI

Polisi waliokuwa wamevalia mavazi ya kawaida wamewakamata makumi ya waandamanaji katika mitaa ya Nairobi huku baadhi ya Wakenya wakiandamana kupinga Mswada wa Fedha wa 2024.
Wakenya waliojaribu kukusanyika nje ya Kituo cha Kitaifa, Hifadhi ya Kitaifa, Kencom na uwanja wa Jeevanjee pia wamekamatwa
Mswada wa Sheria ya Fedha umezua malalamiko makubwa ya umma, huku wakosoaji wakisema kuwa utaweka mzigo wa kifedha usiofaa kwa raia ambao tayari wanakabiliana na matatizo ya kiuchumi.
Imetayarishwa na Janice Marete