#Football #Sports

FANYIA KIKOSI MABADILIKO LAMPARD ASEMA

Huku kikosi cha England kikijiandaa kumenyana dhidi ya Denmark katika mchuano wao wa pili wa makundi kwenye michuano ya Euro 2024, lejendari wa zamani wa kikosi hicho na klabu ya Chelsea Frank Lampard ametoa wito kwa kocha Gareth Southgate kufanya badiliko moja kwenye kikosi.

Lampard amemtaka Southgate kufanya badiliko la kumuanzisha kinda Kobbie Mainoo katika nafasi aliyocheza Trent Alexander Arnold kwenye kiungo cha kati katika mechi ya ufunguzi dhidi ya Serbia.

England kwa sasa wako kileleni mwa Kundi C kufuatia ushindi wao wa 1-0 dhidi ya Serbia Jumapili usiku na watajihakikishia nafasi yao ya kutinga hatua ya mtoano kwa ushindi mwingine dhidi ya Denmark, ambao walitoka sare ya 1-1 na Slovenia katika mchezo wao wa ufunguzi.

Wakati huohuo Wenyeji Ujerumani wamekuwa timu ya kwanza kufuzu kwa awamu ya muondoano ya Euro 2024 Jumatano kutokana na ushindi wa 2-0 dhidi ya Hungary, huku matumaini ya Croatia kusonga mbele yakiwa yamekwama baada ya kufungwa na Albania.

Imetayarishwa na Nelson Andati

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *