#Football #Sports

MATILI WABEBA USHINDI

Timu ya soka ya Matili TTI ilishinda Ligi ya FKF Kanda ya Magharibi kwa msimu wa 2023/24, kwa kuwalaza APS Seal 4-3 kwa mikwaju ya penalti Jumapili katika uwanja wa Shule ya Upili ya Kakamega.

Mchezo huo ulikuwa na ushindani mkali, ambapo kipindi cha kwanza kilimalizika kwa sare tasa licha ya mashambulizi ya pande zote mbili.

Matili TTI,  chini ya kocha Noah Wakhungu, walifunga bao la kwanza kwa winga Hosea Malale.

AP Seal walisawazisha dakika 13 baadaye kwa kichwa kutoka kwa David Olaka na kufanya matokeo kuwa sare ya 1-1.

Allan Muhando, Mwenyekiti wa FKF Kakamega na mwanachama wa kamati ya kandanda ya eneo la Magharibi alipongeza timu zote mbili kwa kile alichokiita onyesho maridadi la kandanda.

Timu zilizofuzu kwa FKF Divisheni ya Pili ni pamoja na APS Seal iliyomaliza kileleni katika Kanda A kwa alama 50, Chuo Kikuu cha Masinde Muliro kilichomaliza alama moja nyuma ya APS Seal, Bukura All-stars, na Matili TTI kutoka Kaunti ya Bungoma.

Chuo Kikuu cha Masinde Muliro kilitoa mfungaji bora, Morphat Otieno, mwenye umri wa miaka 22 akifunga mabao 18 katika mechi 22.

Imetayarishwa na Nelson Andati

MATILI WABEBA USHINDI

KENYA LIONESS WALEMEWA NA CHINA

MATILI WABEBA USHINDI

GOR MAHIA WATAWAZWA WASHINDI WA LIGI KUU

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *