#Football #Sports

MARA SUGAR WALAMBA SUKARI YA USHINDI

Klabu ya Soka ya Mara Sugar imetawazwa rasmi kuwa mabingwa huku pazia la FKF National Super League (NSL) msimu wa 2024  hapo jana , katika uwanja wa Police Sacco licha ya kushindwa kwa bao 1-2 na Vihiga Bullets katika mchezo wao wa mwisho wa Ligi Kuu ya Kitaifa Jumapili jioni,

Denilson Imbayi alianza kuifungia Vihiga Bullets dakika ya 30, huku Mara wakisawazisha dakika ya 60 kwa bao la David Owino.

Kocha wa Mara Sugar, Benedict Wanjala alipongeza timu hiyo kwa ubingwa licha ya kufunga msimu kwa matokeo ya kushindwa.

Wakati huo huo, Naivas FC ilimaliza msimu katika nafasi ya tatu, kufuatia ushindi wao wa 0-1 dhidi ya SS Assad, hivyo kukata tiketi ya mchujo dhidi ya timu ya Ligi Kuu ya Kenya, Sofapaka FC iliyomaliza nafasi ya 16 wiki jana.

Washindi wa pili Mathare United waliilaza Mombasa Stars 2-0 kuashiria kurejea kwao Ligi Kuu kwa mtindo, huku Migori Youth wakiizamisha Rainbow FC 3-0 katika msimu mwingine wa mwisho.

Jijini Mombasa katika uwanja wa Serani, Mombasa Elite walilazimishwa sare moja na Mulembe United na kunusurika katika Ligi Kuu ya Taifa (NSL) msimu ujao.

Kocha mkuu wa Mombasa Elite Patrick Nyale alifurahi kwa kubakiza Mombasa Elite kwenye NSL licha ya kulazimika kupigana hadi siku ya mwisho.

Imetayarishwa na Nelson Andati

MARA SUGAR WALAMBA SUKARI YA USHINDI

NAKHUMICHA ASEMA MSWADA UMEATHIRI SHIF

MARA SUGAR WALAMBA SUKARI YA USHINDI

KENYA NDO WASHINDI WA KABADDI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *