RAIA AWAJERUHI WATATU KWA RISASI

Watu watatu wamepigwa risasi na kujeruhiwa na raia mmoja wakati wa maandamano jijini Mombasa.
Imearifiwa kuwa raia huyo amekasirishwa na waandamanaji waliokuwa wamelemaza shughuli za biashara ndipo akaamua kuwafyetulia risasi kwenye barabara ya Nyerere.
Wakati wa maandamano hayo, mkahawa mmoja wa kifahari umevamiwa, huku waandamanaji wakimsaka raia huyot.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa