#Local News

RUTO AAGIZA TANGAZO LA SRC KUANGAZIWA

Rais William Ruto ameiagiza hazina ya kitaifa kuangazia upya tangazo la tume ya kuratibu mishahara ya wafanyakazi wa umma kutaka kuwapandisha mishahara wafanyakazi wa ngazi ya juu serikalini.

Katika taarifa, rais amesema amehimiza idara zote za serikali kuendesha shughuli zao kulingana na hali ya uchumi nchini na kubana matumizi yao baada ya kutupiliwa mbali mswada wa fedha wa mwaka 2024.

Katika nyongeza hiyo ambayo ilianza kutekelezwa kuanzia Julai moja, mkuu wa mawaziri ataongezwa mshahara kutoka shilingi elfu 957,000 hadi 990,000, huku makatibu wakuu, inspekta mkuu wa polisi miongoni mwa maafisa wengine pia wakipandishwa mishshara.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

RUTO AAGIZA TANGAZO LA SRC KUANGAZIWA

JALANG’O AOGOPA ‘MTEGO’

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *