NAFUU YA AFYA POKOT

Huduma za afya zinatarajiwa kuimarika katika kaunti ya West Pokot baada ya serikali ya kaunti hiyo kuboresha miundomsingi kwenye vituo mbali mbali vya afya.
Nyingi za vituo hivyo ni vya maeneo ya mashinani, serikali ikisema hatua hiyo inalenga kupunguza gharama na changamoto za uchukuzi.
Nao wakazi wa kaunti hiyo wameitaka serikali ya kitaifa kuongeza mgao wa afya ili kuboresha shughuli za matibabu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa