OTIENDE AMOLLO KUONGOZA MISHENI YA WAANGALIZI WA UCHAGUZI NCHINI UINGEREZA

Mbunge wa Rarieda Otiende Amollo ametangaza kuwa ataongoza Misheni ya Waangalizi wa Uchaguzi nchini Uingereza ambayo inatazamiwa leo hii.
Amolo amekaribisha fursa ya kuongoza misheni hiyo ambayo inajumuisha majimbo na wilaya 19 zikiwemo Kenya, Malawi, St Lucia, Jimbo la Alderney, New South Wales, Seychelles, Trinidad na Tobago, Bunge la Jimbo la Jersey na Grenada.
Nyingine ni pamoja na Sri Lanka, Bunge la Turks na Caicos, Malta, Lesotho, Mauritius, Bunge la Kitts & Nevis, Jimbo la Majadiliano, Guernsey, Bunge la St Lucia, Bunge la Anguilla na Uingereza.
Imetayarishwa na Janice Marete