RUTO AZUNGUMZA NA MKUU WA IMF BAADA YA KUONDOA MSWADA WA FEDHA

Rais William Ruto amezungumza na Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Kristalina Georgieva siku chache baada ya kuuondoa Mswada wa Fedha wa 2024 Mswada wa fedha uliojumuisha ongezeko la ushuru ulikuwa msingi wa mageuzi ya sera yaliyokubaliwa na nchi na IMF kama sehemu ya mpango wa ukopeshaji wa thamani ya dola bilioni 3.6.
Mmoja wa wanadiplomasia hao alisema serikali inapaswa kuonyesha dhamira ya kupunguza matumizi mabaya ya fedha, kukabiliana na rushwa na kuongeza uwajibikaji ili kubadilishana na mabadiliko hayo.
Imetayarishwa na Janice Marete