#Local News

VITAMBULISHO, VYETI VYA KUZALIWA TAYARI KUCHUKULIWA

Wakenya waliotuma maombi ya kupata vitambulisho, Leseni za Kuendesha Magari Mahiri na Cheti cha Kuzaliwa wamehimizwa kutembelea Vituo vya Huduma center ili kuchukua stakabadhi zao.

Katika notisi ya jana Ijumaa, Huduma Center ilifichua kuwa vitambulisho elfu 134,602 vya Kitaifa viko tayari kuchukuliwa katika Vituo vyote 53 vya Huduma center kote nchini.

Vyeti vya kuzaliwa elfu 38,928 na leseni 45,575 za udereva pia ziko tayari kukusanywa.
Zaidi ya hayo, Huduma Kenya imesema kuwa utoaji wa leseni za udereva wa bayometriki utapatikana katika vituo 15 vya Huduma center kote nchini.

Vituo vilivyochaguliwa ni GPO, Kibra, Mombasa, Nyeri, Embu, Meru, Kakamega, Eldoret, Thika, Kericho, Nakuru, Kisii, Kisumu, Garissa na Machakos

Imetayarishwa na Janice Marete

VITAMBULISHO, VYETI VYA KUZALIWA TAYARI KUCHUKULIWA

PESA ZA AFISI ZETU ZIKO WAPI? MCA

VITAMBULISHO, VYETI VYA KUZALIWA TAYARI KUCHUKULIWA

X-SPACE YA RUTO NA GEN Z HAIJASHAURIWA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *