EQUITY HAWKS WAFUZU KWA FAINALI

Equity Hawks ilifuzu kwa fainali ya Ligi Kuu ya Kitaifa ya Wanawake ya Mpira wa Kikapu ya Kenya kwa ushindi wa 3-2 dhidi ya Zetech Sparks Jumapili kwenye Ukumbi wa Nyayo Gymnasium.
Wanabenki waliwacharaza wanafunzi 61-46 katika Mchezo wa Tano kati ya mfululizo wa michezo mitano.
Equity itamenyana na mabingwa watetezi Mamlaka ya Bandari ya Kenya (KPA) katika fainali itakayoanza wikendi ijayo.
Zetech walianza mchezo kwa kasi kwa kushinda robo ya kwanza kwa raha 21-09 lakini matumaini yao hayakutimia matarajio yao kwani Equity iliunguruma katika robo ya pili ikishinda 19-07 mchezo ulipoenda mapumziko na alama zikibaki 28 Juu.
Maryann Nyagaki, Betty Kananu na Jemimah Knight walidondosha kwa jumla ya pointi 34 kwa Wanabenki huku Naomi Bosibori akiwa kinara wa Zetech akidondosha pointi 16 huku Maureen Bosibori akiongeza 12.
Kocha mkuu wa Equity Hawks Benson Oluoch aliwapongeza wasichana wake kwa kazi nzuri kwa ufanisi wao.
Imetayarishwa na Nelson Andati