#Football #Sports

DE LA FUENTE AMEZEA USHINDI KATIKA NUSU FAINALI YA EURO

Kocha wa Uhispania Luis de la Fuente ana imani na kikosi chake watakapo menyana na Ufaransa katika nusu fainali ya Euro 2024 hii leo.

Huku wakiwa na wimbi la ushindi mara tano mfululizo, Uhispania wamemulika mchuano huo, wakifunga mabao 11 kwenye njia ya kutinga nusu fainali.

Ufaransa wamefikia hatua hiyo licha ya kukosa ustadi wa kushambulia na bado hawajafunga bao kutokana na mchezo wa wazi. Mabao matatu ya Ufaransa yametokana na penalti moja na mabao mawili ya kujifunga wenyewe.

Mbappe na fowadi mwenzake Antoine Griezmann wamekashifiwa kwa kushindwa kufanya vizuri, lakini de la Fuente alisalia kuwa makini, hasa na nahodha huyo wa Ufaransa.

Kiungo wa kati wa Uhispania Rodri alisema hasikilizi lawama za fowadi huyo wa Ufaransa, anayechukuliwa na wengi kuwa mchezaji bora zaidi duniani.

Katika nusu fainali nyengine ha[po kesho nertherlands watakua wanamenyana nan england kuanzai saa nne usiku masaa ya frika mashariki.

Imetayarishwa na Nelson Andati

DE LA FUENTE AMEZEA USHINDI KATIKA NUSU FAINALI YA EURO

ZETECH WAPANIA KUBEBA LIGI YA VIKAPU

DE LA FUENTE AMEZEA USHINDI KATIKA NUSU FAINALI YA EURO

TAASISI ZA UMMA ZATAKIWA KUPUNGUZA MATUMIZI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *