KARUA ATOFAUTIANA NA RUTO, RAILA

Kinara wa Narc Kenya Martha karua amepuzilia mbali hatua ya Rais William Ruto na kinara wa Azimio Raila Odinga kuitisha mazungumzo ya kujadili masuala ya yanayolikumba taifa, akisema hatua hiyo inalenga kuzima juhudi za vijana wa Gen Z kuleta mageuzi nchini.
Kulingana na Karua, mazungumzo yatakuwa na umuhimu iwapo wahusika wanafanya hivyo kwa nia njema na wanaongozwa na maslahi ya wananchi.
Wakati uo huo, kinara mwenza wa DAP-K Eugene Wamalwa, amesema hakubaliani na wito wa majadiliano.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa