MIGORI: UOKOAJI WA MANSURA UNAENDELEA

Naibu Kamishna wa kaunti ndogo ya Rongo kaunti yam IGORI George Matundura, amesema kwamba shughuli za uokoaji zinaendelea baada ya watu 18 waliokuwa wakichimba migodi katika eneo la Rongo kufunikwa na mgodi huo.
Akithibitisha maafa hayo, Matundura amesema mkasa huo uliotokea majira ya saa saba usiku umewaua watu 5.
Aidha, ameahidi kwamba serikali itaweka mikakati ya kuimarisha usalama wa shughuli za uchimbaji migodi eneo hilo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa