USHURU MTALIPA, MAHAKAMA

Wakenya wataendelea kulipa ushuru wa nyumba za bei nafuu baada ya jopo la majaji watatu wa mahakama kuu kukataa kusitisha kwa muda ushuru huo kutokana na kesi iliyowasilishwa mahakamani.
Kwenye uamuzi wao, majaji hao wamesema kusimashwa kwa ushuru huo hakutakuwa sawa kwa umma, wakisema walalamishi ambao ni seneta wa Busia Okiya Omutatah na wengine 7 hawana Ushahidi wa kuwashawishi kusimamisha makato hayo.
Hata hivyo, majaji hao wameagiza kwamba kesi hiyo isikilizwe kwa haraka ili uamuzi kamili uweze kutolewa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa