17 WAFARIKI KWENYE AJALI TOFAUTI

Watu 17 wameaga dunia kwenye ajali tatu tofauti katika maeneo tofauti nchini, 10 kati yao wakiaga dunia kwenye ajali ya Katumba kwenye barabara kuu ya Mwingi kuelekea Garissa.
Kamanda wa polisi eneo hilo Ifraim Karani amesema majeruhi 11 wanaendelea kutibiwa huku wakirifiwa kuwa katika hali mahututi baada ya basi lililokuwa likielekea Nairobi kuganga trela lililokuwa limeegeshwa.
Katika ajali nyingine, watu watano wamefariki katika eneo la Maragua kaunti ya Murang’a baada ya lori kuligonga gari dogo.
Kwenye ajali ya tatu, mwanamke mmoja na binti yake wamefariki papo hapo katika eneo la Kangundo kaunti ya Machakos kufuatia bodaboda waliokuwa wakisafiria kugongwa na lori.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa