WANAHARAKATI MAHAKAMANI WAKITAKA BUNGE LIVUNJWE

Wanaharakati Peter Agoro, Anthony Wachira na Augustine Muthiani wamewasilisha kesi mahakamani wakitaka mahakama iamuru kwamba bunge la kitaifa ni haramu na lipo kinyume na sheria kufuatia hatua ya bunge hilo kufeli kuafikia sheria ya kijinsia.
Watatu hao wanasema kwamba wanachama wa bunge hilo kwa sasa hawaafikii vigezo vya sheria katika kuhakikisha usawa katika nafasi za uongozi ilivyo kwenye vipengee vya 26, 27 na 81 vya katiba.
Kwenye kesi ambako washtakiwa ni tume ya IEBC, Bunge la kitaifa na mwanasheria mkuu, walalamishi aidha wanaitaka mahakama IEBC kuandaa uchaguzi mdogo katika eneo bunge la Banisa ambako mbunge wao alifariki mwezi Machi mwaka jana.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa