#Local News

JINSI KHALISIA ALIVYOANZA KUWAUA WANAWAKE

Mkurugenzi wa idara ya upelelezi DCI Mohammed Amin amefichua kwamba chanzo cha mshukiwa mkuu wa mauaji ya Kware Collins Jumaisi Khalisia kuwaua wanawake 42 ni wakati ambapo mkewe mshukiwa huyo alifuja pesa za biashara alizofunguliwa na mshukiwa ndipo akaingiwa na hasira na kumwua.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Amin amesema kuwa hatua hiyo ilimsababisha mshukiwa kuingiwa na machungu na kumkatakata mkewe, na kisha ukawa ndio mtindo wake na mara nyingi akiwapendelea sana wanakwake waliokuwa warembo machoni pa mshukiwa.

Amin amesema mshukiwa amekamatwa baada ya uchunguzi wa kina uliofanywa kwa simu ya mmoja wa waathiriwa.

Kwa upande wake, kaimu Inspekta Mkuu wa polisi Douglas Kanja, Jumaisi mwenye umri wa miaka 33 amesema amenaswa akiwa mtaani Kayole akiwa na mwili wa mwanamke uliokuwa ndani ya gunia, tayari kuutupa.

Imetyarishwa na Antony Nyongesa

JINSI KHALISIA ALIVYOANZA KUWAUA WANAWAKE

KESI DHIDI YA GACHAGUA YAONDOLEWA MAHAKAMANI

JINSI KHALISIA ALIVYOANZA KUWAUA WANAWAKE

UTEUZI WA MWAURA KRA WABATILISHWA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *