HALI YA MAANDAMANO NCHINI

Hali ya taharuki imetanda katika mengi ya maeneo nchini huku biashara nyingi zikifungwa kufuatia maamndamano ya vijana wa kizazi cha Gen Z.
Jiji Nairobi, waandamanaji wamefunga barabara ya Moi Avenue karibu na eneo la Kencom katikati mwa jiji kwa kutumia mawe, polisi wakilazimika kuwatawanya kwa vitoza machozi.
Jijini Nakuru, waandamanaji wanaendeleza mchezo wa paka na panya na maafisa wa polisi, hali sawa ikishuhudiwa jijini Mombasa na Kisumu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa