AUSTRALIA YAMNYAKUA MATHEW RYAN

AS Roma imemsajili mchezaji wa kimataifa wa Australia Mathew Ryan, kama mchezaji huru kwa mkataba wa msimu mmoja na chaguo la mwaka mmoja zaidi.
Kipa huyo mwenye umri wa miaka 32 amesajiliwa kama msaidizi wa kipa chaguo la kwanza Mile Svilar katika timu HIYO ya KOCHA Daniele De Rossi.
Anajiunga na Roma baada ya kuACHILIWA HURU NA AZ Alkmaar mwishoni mwa msimu uliopita.
Ryan ameichezea Australia mara 93 na aliichezea Socceroos katika Makala tatu za Kombe la Dunia.
Imetayarishwa na Nelson Andati