WAFANYABIASHARA WEBUYE ‘WAHOFIA’ MAENDELEO
Wafanyibiashara katika soko la dina mjini Webuye sasa wanaitaka mamlaka ya barabara nchini KENHA kusitisha ubomozi wa maduka yaliyo karibu na barabara kuu ya Misikhu kuelekea Webuye, wakisema iwapo shughuli hiyo itaendelea huenda ikaathiri mapato yao ya kila siku.
Wakizungumza na wanahabari mjini Webuye,wafanyibiashara hao wakiongozwa na mwenyekiti wao Abel Wanjala na katibu Rachael Khaemba, wamesema mapato yao ya kila siku hutegemea maduka na vibanda hivyo na ubomozi huo huenda ukawaathiri pakubwa.
Aidha, wamedai kuwa soko la Dina ni mmoja wapo ya masoko katika kaunti ya Bungoma yanayochangia pakubwa kwa pato la kaunti ya Bungoma, wakimtaka gavana Ken Lusaka kuingilia kati.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































